WELCOME TO MY BLOG AND HAVE FUN...You can Translate to any language you want by clicking TRANSLATE on the side..
Jul 25, 2012
NDANI YA CHADEMA LEO.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepokea wanachama wapya 256 kutoka vyama vya CCM, Cuf, na TLP kutoka katika Kata nne za Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Hayo yalibainishwa na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kilombero , Moses Kisenime katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Kisenime alisema wanachama hao walipokelewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Bavicha), John Heche wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara jimboni humo.
Alisema Mwenyekiti huyo wa Bavicha taifa aliwapokea wanachama hao katika mikutano minne aliyofanya katika Kata ya Ifakara, Mang’ula, Msolwa na Mkamba.
“Kutokana na mikutano yetu tunayoifanya mkoani Morogoro tumeweza kupokea wanachama 214 kutoka CCM, Cuf 28 na TLP wanachama 14,” alisema Kisenime.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake aliyekuwa balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mkamba, Mussa Katanduki alisema ameamua kuhama kutoka chama cha CCM kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mueleko na maadili ya uongozi.
“Sijalazimishwa na mtu kuhamia Chadema lakini kutokana na mambo yalivyo ndani ya CCM kwa ihari yangu nimeamua kuungana na chama hiki ili kuweza kuendeleza mapambano ya kutetea haki za wanyonge,” alisema Katanduki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment