CHOMA MAHINDI, KAANGA KARANGA DO SOMETHING BASI,,,,
Kujituma ni jambo zuri sana miongoni mwa binadamu, wapo watu hii leo ambao hulalamika ugumu wa maisha ilihali hawafanyi shughuli yeyote ya kujiingizia kipato au kujipatia ridhiki.
Wanawake wengi katika miji mikubwa hapa nchini
wamekuwa ni watu wa kukaa majumbani tu iwapo wamekosa kazi za kuajiriwa
maofisini jambo ambalo linapelekea kupachikwa majina mbalimbali ikiwapo lile la
UGOLI KIPA.
Kwanini uitwe Goli kipa huku zipo shughuli mbalimbali
ambazo wewe zinaweza kukupatia kipato na ukaweza ama kuendesha maisha yako na
kujiepusha na vitendo vibaya au hata kujipatia fedha ndogo ndogo za mahitaji
yako binafsi.
Daima kushinda majumbani kwa wanawake wengi wasio
penda kujiajiri na kujishughulisha na vitu vidogo vidogo kama kuuza karanga,
kuchoma mahindi, vitumbua na maandazi, husababisha wanawake hawa kuwa na majungu
na mambo mengi ya Umbea.
Baadhi yao wanasema kujishughulisha kunawafanya kujiepusha na makundi yanayoendekeza umbea mitaani na kusengenyana, lakini pia kuisaidia familia na wao wenyewe kuepuka kuwa omba omba hata kwa mafuta ya kujipaka.
Pichani ni
mwanamke mkazi wa Jijini Arusha akijishughulisha na uuzaji wa Karanga, biashara
ambayo inamuingizia kipato japokuwa ni kidogo lakini anaweza kumudu maisha yake
na kuongeza pato la familia wakati baba amekwenda katika shughuli
nyingine.
Blog inachukua fursa hii kumtaka mwanamke yeyote ambaye ana uwezo wa kufanya kitu pale alipo na aanze sasa kufanya hivyo. Ipo dhana ya kusema Mwanamke akiwezeshwa anaweza lakini ukweli ni kuwa mwanamke akijituma anaweza hebu anza sasa na utaona matunda yake, na waala usitake mtaji wa kuanza duka la vipodozi au nguo kama jirani yako.
No comments:
Post a Comment