UJIO HUU LAZIMA WAKIMBIE.
Star wa muziki wa kizazi kipya Bongo Dogo Janja 'Janjaro' anayewajibika ndani ya kundi maarufu la Mtanashati linalokuja kwa kasi kubwa hivi sasa kwenye game ya Bongo Fleva likiwa chini ya Ostaz Juma na Musoma amesema kuwa kutoka kwa singo yake mpya aliyoibatiza jina la 'Ya Moyoni' ni ujio mpya ambao utawafanya wapinzani wake kukimbia.
Akizungumza na Teentz.com mapema leo Dogo janja amefunguka kuwa anataka kuwahakikishia mashabiki wake kuwa kuondoka kwake ndani ya kundi alilokuwa akilitumikia hapo awali kulikuwa ni kwa chuki zilizoibuka baada ya kuanza kudai haki zake.
"Huu ni ujio wa nguvu za ajabu, naajua watakimbia, kwani siku zote mtu huwezi kuhukumiwa kwa kudai chako naomba mashabiki wanipokee kwa mara nyingine kwani sasa niko chini ya amtu anayejua nini maana ya kipaji na pia anajua kuhusu maslahi ya mtu" alisema Dogo Janja.
Katika hatua nyingine bosi wa kundi hilo Ostaz Juma na Musoma ameiambia Teentz.com kuwa wameachia ngoma ya pamoja ambayo imewajumuisha nyota wote wanaounda kundi hilo na kuipachika jina la 'WATASUBIRI'
No comments:
Post a Comment