Apr 15, 2013





Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema ameamua kuweka wazi ndoto yake hiyo ya miaka mingi ambapo ilikuwa kuitumikia jamii ya Kitanzania.
“Nimeamua kuweka wazi kwamba mwaka 2015 nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda muafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii,” alisema JB.
Hata hivyo, ‘mheshimiwa’ huyo hakuwa tayari kuanika ni jimbo gani atagombea akisema atatangaza baadaye licha ya kudai kwamba ni jimbo moja kubwa lenye upinzani mzito kila ukifika wakati wa uchaguzi.
“Nasisitiza nitagombea, lakini siwezi kuweka wazi ni jimbo gani, hilo nitaliongelea baadaye, ila ni kubwa lenye upinzani mkubwa kila wakati wa uchaguzi,” alisema JB.

No comments:

Post a Comment