Apr 19, 2013

Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ si mtoto tena, ametimiza rasmi umri wa miaka 18, kilichofuata ni kuangusha bonge la pati ya bethidei....



Lulu ambaye hivi karibuni aliachiwa kwa dhamana katika kesi ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba aliangusha pati hiyo katika hoteli ya nyota tano ya Serena ya jijini Dar usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, Aprili 17, mwaka huu.
MAMA LULU NDANI
Shushushu wetu aliyekuwa ndani ya sherehe hiyo alinyetisha kuwa ilihudhuriwa na watu maalum wachache wakiwemo rafiki, wasanii na mama yake mzazi, Lucresia Karugila.
TUMSHUKURU MUNGU
Ilinyetishwa kwamba kabla ya yote, wageni waalikwa waliokuwa na nyuso za furaha walishirikiana na familia ya Lulu kumshukuru Mungu na kumwomba amzidishie staa huyo umri wa kuishi duniani bila vikwazo vya shetani.
“Kikubwa ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa kumfanikisha kufikisha umri wa miaka 18 kwani huko nyuma kulikuwa na maneno mengi juu ya umri wake,” alinyetisha mtu wetu.
NENO LA LULU
Muda mfupi akiwa ukumbini hapo, Lulu alitundika picha za tukio hilo kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika: No more questions (hakuna maswali zaidi)…No more answers (hakuna maji zaidi)…No more lies (hakuna uongo zaidi).
Katika moja ya keki za zoezi hilo kulikuwa na maandishi yaliyosomeka: Happy birthday Lizy “official 18”. Katika sentensi nyingine, maandishi hayo yalimaanisha kuwa amefikisha rasmi miaka 18.
MISOSI, VINYWAJI
Chanzo hicho ambacho
kilifuatilia pati hiyo hatua kwa hatua kilinyetisha kuwa kulikuwa na misosi na vinywaji vya kumwaga ambapo wahudhuriaji walikula na kunywa hadi wakasaza.
LULU MNG’ARO
Kwa macho ya kawaida kabisa, Lulu aling’ara sawia ndani ya gauni refu jeupe lenye kuacha mgongo wazi na kiatu kirefu cha ‘CL’.
“Yaani kiukweli pati ya Lulu ilikuwa bab’kubwa, kwanza ilikuwa ni ya kistaarabu mno na watu wote walipendeza sana akiwemo Lulu mwenyewe. Haikuwa ya kihuni kama wafanyavyo mastaa wengine,” alisema  mpashaji wetu.


No comments:

Post a Comment