Wasamaria wema wakitoa msaada kwa wanafunzi wa shule ya St Chalresy Iringa waliojeruhiwa katika ajali leo
Wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali wakilia kwa uchungu kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Wanafunzi hao wakiwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Askari wa usalama barabara wakifika eneo la tukio kutoa msaada
Wanafunzi hao majeruhi wakiwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Askari wa usalama barabarani akitoa msaada kwa majeruhi wanafunzi wa St. Chalresy leo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
WANAFUNZI zaidi ya 20 wa shule ya kimataifa ya St Charles iliyopo Don Bosco katika Manispaa ya Iringa wamenusurika kifo baada ya gari waliyokuwa wamepanga aina ya Daladala lenye namba T415 AEG kushindwa kupanda mlima na kupinduka.
Huku mbinu za wezi wa watoto zikionyesha kugonga mwamba baada ya mwanamke mmoja kushtukiwa akitaka kukimbia na mtoto asiye wake kwa madai anamkimbiza Hospitali.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 mchana wa leo katika eneo la Msikiti wa Hidaya katika kata ya Mvinjeni katikati ya mji wa Iringa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio baadhi ya mashuhuda walisema kuwa daladala hilo ambalo lilikuwa likitokea eneo la Frelimo katika Manispaa ya Iringa kuelekea mjini Iringa mara baada ya kufika eneo hilo lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma kwa kasi kabla ya kupinduka.
Alisema shuhuda huyo Juma Omari kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ,ubovu wa gari hilo pamoja na uzembe wa dereva ambaye alionekana kuendesha gari hilo kwa bila kuchukua tahadhari na pamoja na kutambua mbele kuna kona na mlima ila hakuweza kuzingatia hilo.
Hata hivyo alisema kutokana na ajali hiyo dereva na konda wake waliwatelekeza watoto hao ambao wanakadiliwa kuwa na umri wa miaka 7 na 9 na wao kutoweka kusikojulikana na kuwaacha watoto hao bila kuwapa msaada wowote hadi wananchi walipofika kutoa msaada wa kuwatoa katika daladala hilo na kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi .
Alisema katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya mwanamke mmoja ambae jina lake bado kufahamika aliyejeruhiwa vibaya mikono yake.
Hata hivyo mmoja kati ya wauguzi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa ambae hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa Hospitali hiyo alisema kuwa hali za watoto hao si mbaya sana zaidi ya kupata michubuko midogo midogo .
Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwapongeza wananchi wa kata hiyo ambao walifika kutoa msaada kwa watoto hao kwa kuwakimbiza Hospitali.
wakati huo huo mwanamke mmoja ambae jina halikuweza kupatikana mara moja amedaiwa kutka kuiba mmoja kati ya watoto waliojeruhiwa kwa madai kuwa ni mtoto wake na alikuwa akitaka kumkimbiza Hospitali ya wilaya ya Iringa Frelimo badala ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa ambako majeruhi wengine walikimbizwa .
Mwanamke huyo alishtukiwa baada ya kukutwa akitimua mbio uchochoroni huku akiwa na mtoto huyo na baada ya kubanwa aliamua kumtelekeza mtoto huyo na kukimbia hali iliyopelekea uongozi wa mtaa kuomba watoto wote wale waliojeruhiwa na wazima kukimbizwa Hospitali ya mkoa .
No comments:
Post a Comment