Apr 15, 2013

WABUNGE KUPITIA MRADI WA UNDP (LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT) WAPEWA SOMO KUHUSU CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI ALBINO


Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa Legislative Support Project, imeandaa semina ya kuwapa Uelewa waheshimwa Wabunge kuhusu Changamoto zinazowakabiri Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albinism) ili kuwa na uwelewa mpana kuhusu changamoto zinazowakabili albino. Semina hii ni mwendelezo wa semina za kutoa elimu kwa waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Ofisi ya Bunge kupitia Mradi wa Legislative Support Project, ambao upo chini ya Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) ili kuwajengea wabunge na watumishi katika kutekeleza majukumu yao ya Kibunge, hususani, uwakilishi wa wananchi pamoja na kuisimamia na kuishauri serikali.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Margareth Sitta (MB) akitoa neno la Utangulizi wakati wa Ufunguzi wa Semina hiyo jumamosi
 Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Nchini Ndg. Ernest Kimaya akitoa utambulisho kwa baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Maalbino waliofika katika Semina hiyo.
 Mwakilishi wa Mradi wa Legislative Support Project uliochini ya UNDP Bi. Anna Hovhannesyan akitoa maelezo mafupi kuhusu Mradi wa Legislative Support Project kwa Waheshimiwa Wabunge
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifafanua baadhi ya changamoto zinazowakabiri maalbino kabla ya kumkaribisha  Waziri Mkuu kufungua rasmi Semina hiyo.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akifungua rasmi semina kuhusu Changamoto zinazowakabiri Maalbino kwa waheshimiwa wabunge katika Ukumbi wa Msekwa, Dodoma.
 Mbunge wa Lindi Mjini Mhe. Salum Barwani ambaye nae ni mlemavu wa ngozi akitambulishwa katika semina hiyo.
Washiriki wengine wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
 Mwakilishi wa Mradi wa Legislative Support Project uliochini ya UNDP Bi. Anna Hovhannesyan akiteta jambo na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa Semina hiyo jumamosi.

No comments:

Post a Comment