Jul 31, 2012

BAADA YA UZUSI KUWA AMEFARIKI,,,

DK. ULIMBOKA SI WA LEO WALA

Dk. Steven Ulimboka.

Hali ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, inaendelea vizuri lakini si wa kupona leo wala kesho, imeelezwa na vyanzo vyetu.
Dk.Ulimboka anayetibiwa Afrika Kusini, yupo chini ya uangalizi mkali wa madaktari katika hospitali aliyolazwa na wanafanya kazi kubwa kuhakikisha anapona.
Chanzo chetu kimetoa taarifa kuwa, Dk. Ulimboka anapata matibabu sahihi kwa sababu hospitali aliyolazwa ni ya uhakika.
Awali, kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja kwenye simu, ripota wetu alimtumia SMS mtoa habari wetu kumuulizia maendeleo ya daktari huyo naye akajibu: “He’s recovering slowly.” (Anapona taratibu).
Alipomuuliza Watanzania wamtegemee lini daktari huyo kurudi nchini, alijibu: “Itachukua muda kupona. Muhimu kwa sasa ni Watanzania na wote wanaompenda, wamuombee kwa Mungu ili matibabu yaende sawa.”
VIPI USALAMA WAKE?
Chanzo chetu kilibainisha kuwa usalama wa Dk. Ulimboka ni wa uhakika, kwani watu wanaomlinda hospitalini hapo wapo makini.
“Nani asiyejua mazingira ya hatari aliyonayo Steven (Dk. Ulimboka)? Hii inasababisha maisha yake hospitalini yawe chini ya ulinzi mkali.
“Kwanza si kila mtu anaruhusiwa kwenda kumuona. Hospitali yenyewe aliyolazwa hatutaki itangazwe. Maisha ya Steven ni siri,” alisema mtoa habari wetu na kutoa siri hii:
“Wiki iliyopita pale hospitali alipolazwa, alitokea mtu fulani hivi Mwafrika. Muonekano wake ukawafanya watu wahisi ni Mtanzania. Watu wanaohusika na usalama wa Steven walikuwa makini sana.
“Kilichosababisha yule mtu aonekane ni Mtanzania ni fulana aliyovaa, kifuani ina ramani ya Tanzania. Watu wanaomlinda Steven wakaogopa sana, wakamfuatilia hatua kwa hatua bila mwenyewe kujua. Bahati nzuri naye alikuwa amekwenda kwa shughuli zake na akaondoka salama.
“Kwa kifupi, hali ilivyo pale hospitali ni kwamba ulinzi ni mkali, tena afadhali mtu awe wa taifa lingine, Watanzania ndiyo wanaogopwa zaidi, kwani huwezi kujua nani mzuri wa Steven na adui yake ni yupi.”
TATIZO LILIPOANZIA
Dk. Ulimboka, akiwa kwenye harakati za kuendeleza mgomo wa madaktari ili kuishiniza serikali iridhie madai yao, alitekwa kisha akavunjwa mbavu, miguu yote, kung’olewa meno yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio hilo, linadaiwa kufanywa na watu wasiojulikana ambapo kabla ya kufanyiwa unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kisha kumtelekeza katika eneo la Msitu wa Mabwepande, nje ya Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment