Jul 28, 2012

MACHANGUDOA WACHARAZWA BAKORA NA WAUMINI WA KIISLAMU.....

BAADA YA KUENDELEZA UCHANGUDOA WAKATI HUU WA MWEZI MTUKUFU.....
KINONDONI......
Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega Waislamu. Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona… WATUMIA BAJAJ Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.

No comments:

Post a Comment