Jul 20, 2012

MPATANISHO KATI YA WEMA SEPETU NA JOKATE WAGONGA MWAMBA

JOKATE...
WEMA SEPETU.
KUTOELEWANA kati ya ma-Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (No. 1) na Jokate Mwegelo (No.2) (pichani) kumeendelea kushika kasi na sasa bifu lao lina kila dalili ya kwenda hadi mwisho wa maisha yao, Fashion Detective lishuka na ushahidi wa kutosha. Awali bifu la wawili hao lilidaiwa kuwa chanzo chake kilitokana na Jokate kuunga uhusiano wa kimapenzi na msanii nyota wa Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ huku akijua wazi ana uchumba wake Wema. Uadui ulianzia hapo, Wema akalia sana kupitia vyombo vya habari, lakini mara zote Jokate amekuwa akikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond licha ya kwamba ushahidi wa kimazingira umekuwa ukieleza kwamba wawili hao wanatoka pamoja. Kufuatia hali hiyo, Wema na Jokate wakawa maadui wakubwa huku jamii ikiwatazama kwa macho ya chongo kuhusu uhusiano wao kuharibiwa na kitu mapenzi. Juni 2012, baadhi ya wadau walitupasha kwamba waliandaa mchakato wa kuwaweka chini wawili hao ili kuwapatanisha hata kwa kutumia vitabu vya Mungu ambavyo vina vipengere vinavyoelekeza binadamu kusameheana. Tulianza na Jokate Lengo lilikuwa kwamba akikubali kupatana na mwenzake, Wema naye angeitwa ambapo mazingira yalionesha kupatikana kwake ni rahisi kuliko Jokate. ALICHOKUWA AKIJIBU JOKATE Pamoja na kupigiwa simu wakati mwingine akitumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu ‘SMS’, Jokate akawa anapiga danadana kwa kutoa udhuru wa kawaida. “Nitakuja, kuna mambo nayaweka sawa kwanza, nikishayakamilisha nitakuja, kuna nini kwani?” Paparazi: Kuna mambo ya kuzungumza ya kawaida lakini. Jokate: Oke, nitakuja jamani. Hata hivyo, mpango wa Jokate kupatikana ulishindikana baada ya kuendelea kudai kuna mambo anayaweka sawa kwanza. Ndipo paparazi aliyepewa jukumu la kumsaka staa huyo na kumfikisha kwenye mahojiano hayo kisha aitwe Wema alipoamua kumuwekea wazi modo huyo kuhusu kuwepo kwa mpango wa kuwapatanisha yeye na Wema. Aidha, paparazi alimgeukia Wema ambapo alimpigia simu na kumwelezea ‘ei tu zedi’ kuhusu zoezi la kupatanishwa na hasimu wake Jokate. JOKATE AFUNGUKA “Mimi sitaki kabisa, sitaki kabisa kupatanishwa kwani sina kisirani na huyo mtu (Wema) wala sitaki na siwezi kushindana naye.” MSIKIE WEMA NAYE Wema naye, bila kujua Jokate amejibu nini, aliwaka kama moto wa kifuu akisema: “Siwezi kupatana na Jokate kwa sababu simpendi huyo mtoto hata kabla hajaniibia Diamond wangu. Hata wakiwepo watu wa kutupatanisha, mimi siwezi kumsamehe. “Nilimsamehe Jack (Wolper) kwa sababu watu walikuwa wanatuchonganisha na lile bifu langu na yeye lilikuwa la kisichana tu.”

No comments:

Post a Comment