Jul 26, 2012

MGAMBO MOROGORO WAPATA KIBANO BAADA YA KUCHOMA MOTO VIBANDA VYA MAMA LISHE...

Hivi ndivyo ilivyokuwa.....
Moja ya mabanda ya mama lishe yalivyo teketea..
Paa la Makuti likiteketea moto...
Moto umepamba moto...
WANANCHI wenye hasira jana waliwashushia kichapo  mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro baada ya kuchukizwa na kitendo cha mgambo hao kuwavamia bila taarifa na kuchoma moto mabanda ya biashara ya kina mamantilie (mama lishe)  yaliyokuwa kando  ya barabara ya kuelekea Dar es Salaam eneo  la Area Five jirani na uwanja wa maonyesho ya kilimo ya Nane Nane. Mgambo hao baada ya kuzidiwa nguvu na kundi la wananchi   walilazimika kutimua mbio kunusuru maisha yao na kuviacha baadhi ya vitendea kazi vyao  vyao vikiwemo virungu  na viberiti. Wakizungumza na mtandao huu,  baadhi ya kinamama hao waliochomewa mabanda waliwashutumu mgambo hao kwa kuwavamia bila taarifa na kuchoma moto mabanda yao  na masufuria ya wali na ugali.

No comments:

Post a Comment