Jul 24, 2012

SIASA LEO...

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeingiwa na hofu baada ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutangaza maazimio wanayodai yana utata ndani yake na yenye kuhatarisha amani ya nchi. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho la CCM, Vyuo Vikuu nchini, Bw. Asenga Abubakar, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio yaliyopitishwa na Kamati Kuu ya CHADEMA na kudai baadhi ya vipengele vilivyotolewa na chama hicho vinawapa hofu kutokana na kuwahi kutendeka kwa baadhi ya matukio. “Kuna vipengele vingine wameviongolewa kwenye maazimio yao na sisi vimetupa hofu, hatuelewi nchi inakwenda wapi ni bora CHADEMA ikaweka bayana maazimio haya kwa wananchi. Akijibu tuhuma hizo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, alisema hizo ni njama zinazofanywa na baadhi ya watu kwa kusambaza waraka feki wa chama hicho. Alisema chama hicho kimesikitishwa na kitendo cha kusambazwa waraka ambao umeongezwa baadhi ya maazimio. “Kuna watu wamegushi na kusambaza waraka wakidai ni wa CHADEMA, kuna kauli ambazo si zetu bali za chama fulani, kitendo hiki kinaweza kupoteza amani ya nchi,” alisema. Aliongeza kuwa, katika waraka huo ambao CHADEMA unao, kuna kipengele kinachosema 'Idumu nguvu ya Umma' ambapo chama hicho hakijawahi kutumia kauli ya namna hiyo. “Sisi hatuna kauli ya namna hiyo, hata kwenye karatasi hatuwezi kuandika, kauli yetu ni 'Peoples Power' hii ni fitina na uchochezi katika nchi, tunakanusha kuhusika na waraka huu,” alisema. Wiki iliyopita CHADEMA ilitoa maazimio likiwemo suala la Operesheni Sangara ambayo wataifanya katika mikoa mitano ambayo ni Morogoro, Dodoma, Singida, Manyara, Iringa. Kampeni hiyo imepangwa kuanza wiki ijayo katika majimbo 44, kata 806 na vijiji 4,000.

No comments:

Post a Comment