Jul 23, 2012

USIOMBE YAKUKUTE....













USIOMBE yakukute! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’, Lulu John (mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe (siyo Mr. Nice).
Lulu alidai kumfumania bwana’ke Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina halikupatika kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
FUMANIZI LILIKUWA HIVI;
 Kwa mujibu wa Lulu, akiwa kwenye mihangahiko ya kusaka bingo, alitonywa na mtu wake wa karibu kuwa mumewe Abdulatif yupo kwenye nyumba hiyo ya wageni akiigagadua amri ya sita nje ya mkataba.
Lulu, baada ya kuthibitishiwa kuwa mumewe anacheza ‘nje kapu’ ndipo akakodi bodaboda fasta na kuwahi eneo la tukio kwani naye siyo mgeni wa uwanja huo wa mechi za kitandani.
Alidai kuwa ilimchukua dakika 12 tu kutoka Kijitonyama, Dar anakoishi na mumewe hadi eneo la tukio.
NDANI YA GESTI...
 Aliendelea kusema kuwa baada ya kutinga mahali hapo alikwenda moja kwa zote hadi kwenye chumba walichojichimbia wawili hao na kuanza kubamiza mlango huku akipiga mayowe ya kuomba msaada.
WENGINE WADHANI WAMEFUMANIWA
Huku akizidisha kupiga kelele akitaka kuvunja mlango, ndipo akakatiza stimu za watu wengine waliokuwa wakilimega tunda tamtam kwenye vyumba vingine ambao walitoka kwa kihoro wakidhani wamefumaniwa wao.
MUME ATIMKA NA NGUO YA NDANI
Aliendelea kusimulia mkasa kuwa watu walianza kujaa nje ya chumba hicho ndipo Abdulatif akafungua mlango kwa kasi na kutimka kama mkizi akiwa na nguo ya ndani pekee kisha akaruka fensi.
WATU PIPOOO!!
Alisema kuwa wakati anachomoka nduki alimgonga kikumbo Lulu na kumwangusha chini huku akimwacha akigaragara ambapo watu walikuwa wakimkimbiza wakisema: “Weweee.”
VITA
Baada ya kunyanyuka na Abdulatif kumchomoka hivihivi ndipo vita kuu ikaanza dhidi ya mgoni wake.
AMEGWA PUA
 Alisema kuwa ngumi za uhakika zilipigwa hadi yeye (Lulu) akang’atwa pua ambapo alitokwa na damu chapachapa usoni huku aliyefumaniwa akitafuta njia ya kujisitiri baada ya kuchaniwa nguo na kubaki mtupu.
Baada ya hali kuwa mbaya, Lulu alisema walitokea wasamaria wema na kuwatuliza ambapo yeye alikimbilia Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kumfungulia mgoni wake shitaka la shambulio la kudhuru mwili lenye jalada la kesi namba OB/RB/12675/2012.
Kwa mujibu wa Lulu, kitendo cha kumfumania mwanaume huyo kimemuumiza kwani amekuwa akimtunza kwa hali na mali na hakuweza kuamini kama angeweza kumsaliti.
Juhudi za kumpata Abdulatif zilishindikana ila blog yetu itajitahidi kwa hali na mali kupata utamu huu kutoka kwa mwenyewe Abdulatif.

KWA NINI USIOMBE YAKUKUTE?
Lilikuwa ni tukio la aina yake ambalo halikuishia pale gesti tu bali liliingia mtaani ambapo vitendo vya Abdulatif kukimbia akiwa mtupu na Lulu kung’atwa pua viligeuka gumzo na kila mtu akimuomba Mungu asikutwe na kasheshe kama hilo.

No comments:

Post a Comment