Aug 4, 2012

JACK,UWOYA NDOA ZA MBWEMBWE ZAWATOKEA PUANI

Irene Uwoya.
Jacqueline Patrick.


NDOA zilizotawaliwa na mbwembwe nyingi za Irene Uwoya na Jacqueline Patrick sasa zinawatokea puani kwani wote kwa sasa wako kwenye hatihati ya kukosa heshima ya kuitwa wake za watu, Ijumaa linakudondoshea.
Irene aliolewa na Hamad Ndikumana Julai, 2009, Jack naye aliolewa na Abdullatif Fundikira Desemba 2011 ambapo wote walitumia mamilioni ya fedha huku sherehe zao zikitawaliwa na mbwembwe lakini sasa hivi ndoa zao ziko gizani.
Wakizizungumzia ndoa hizo hivi karibuni, baad
hi ya mashabiki wa mastaa hao walionesha kusikitishwa na yale yanayotokea kwao huku wakiwataka wajiangalie mara mbilimbili.
“Kwa kweli ni aibu, wamefanya sherehe za mbwembwe sana tuka
jua wamedhamiria kuingia kwenye ndoa lakini ona sasa…, Jack ndiyo huyo keshavua pete ya ndoa, Uwoya naye haeleweki, Ndiku kamuacha Bongo,” alisema mama Salmina wa Kinondoni jijini Dar.
Naye Aboubakar Sele
wa Sinza alisema, madhara ya kukurupukia kuingia kwenye ndoa bila kujipanga ndoa yanayowapata mastaa hao kwani inavyoonekana hawakuwa ‘sirias’.
“Kimsingi ndoa zao za kifahari zinawatokea puani sasa, aibu hawawezi kuikwepa, walipoolewa waliteketeza mamilioni ya shilingi lakini leo hii wako gizani,” alisema Abou.
Hata hivyo, wengi walioongea na mwandishi wetu walisema mastaa hao bado wana nafasi ya kuweka mambo sawa hivyo Jack ajirudi kwa mumewe aliye gerezani, Uwoya naye akamuombe msamaha Ndikumana.No comments:

Post a Comment