Aug 8, 2012

KIKOSI KUANDAA FILAMU YA ULIMBOKA

KUNDI la Muziki wa Hip-Hop nchini, Kikosi cha Mizinga, kinatarajia kuandaa filamu itakayohusu tukio la kutekwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka.

Akizungumza na Blog, Kiongozi wa Kikosi cha Mizinga, Kalama Masoud ‘Kalapina’, alisema filamu hiyo ina lengo la kupinga ukatili wa namna hiyo nchini.

“Kutokana na tukio lililomkuta Dk. Ulimboka, Kikosi tumeona bora tutengeneze filamu kuhusiana na tukio hilo ili kupiga vita kitendo hicho na Watanzania tuishi kwa amani,” alisema Kalapina.

Kalapina alisema, katika filamu hiyo, muhusika mkuu atakuwa yeye mwenyewe atakayeigiza kama Dk. Ulimboka na mtekaji atakuwa Van Dame, pamoja na waigizaji wengine.

Alisema kuwa, vipande vya filamu hiyo itapatikana katika video ya nyimbo yake ya Fasihi itakayoanza kurushwa katika vituo vya televisheni hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment