Aug 16, 2012

KOFFI OLOMIDE KIZIMBANI KWA KUMTIA KIBANO PRODUCER WAKE,,,MWANAMUZIKI mahiri barani Afrika, Koffi Olomide ameshitakiwa kwa kumpiga producer wake aliyemwandalia albamu yake mpya ya Abracadabra.
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani jana Jumatano.
Olomide alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.
Mahakama ambapo kesi hiyo ilisikilizwa mjini Kinshasa palifurika kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo ilihairishwa hadi leo asubuhi wakati aliposhitakiwa rasmi.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na prodyuza wake Diego Lubaki, ni kuhusu pesa Euro 3,000.
Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.

No comments:

Post a Comment