Aug 15, 2012

MBIO ZA KONDOO ZAVUTIA MAELFU HUKO SCOTLAND

Kondoo wakishindana kumalizia mbio huko Dumfriesshire, Scotland.

MAMIA ya mashabiki walijaa katika mitaa ya Moffat, Dumfriesshire, nchini Scotland, kushuhudia mashindano ya mbio za kondoo yaliyofanyika katika mitaa ya mji huo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mashabiki wa mchezo huo waliwekeana madau ya fedha ambapo kondoo alitwaye Lingonberry, alishinda.
“Ni mchezo mpya ambao umefanyika mara ya kwanza katika mitaa ya Scotland, na tunategemea kuufanya kila mwaka kwa siku mbili na hatimaye wiki nzima,” alisema Thomas MacDonald, mtayarishaji wa tukio hilo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Moffat Promotions Group.

No comments:

Post a Comment