Aug 27, 2012


MISS EAST AFRICA 2012 KURUSHWA “LIVE” NA M-NETMashindano ya Miss East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa kutizamwa na watu wanaokadiliwa kufikia million 200 kupitia televison na kwa njia ya internet Dunia nzima.
 Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi ambapo yamepangwa kufanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City,  jijini Dare s salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa imetangazwa awali ili kutoa muda zaidi kwa Nchi ambazo hazijapata wawakilishi wao kuweza kukamilisha zoezi hilo.
 Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za ukanda wa afrika mashariki.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
 

No comments:

Post a Comment