JUA KALI AKIWA NDANI YA NDINGA YAKE
Siku chache baada ya kumaliza kugonga kichupa cha wimbo wake mpya, nyota wa hip hop pande za Kenya, Jua Kalli amevuta ndinga mpya ya kisasa aina ya Chrysler Crossfire yenye thamani ya Shilingi za kibongo milioni 70.
Akizungumza VIA 4N na teentz.com kutoka Nairobi Jua kali amefunguka kuwa siku zote amekuwa akivutiwa na kumiliki ndiga sports hasa zinazotengenezwa Ujerumani n akilichotokea sasa ni kama kutimiza ndoto aliyokuwa nayo.
"Maisha yana mambo mengi, lakini nafurahi nimetimiza ndoto yangu, kununua gari hili siyo kwamba mimi ni bora, huu ni utaratibu wa maisha tu ni kitu ambacho mtu mwingine yoyote anaweza kufanya, hata hivyo namshukuru Mungu kwa hatua hii" alisema Jua kali
No comments:
Post a Comment