Aug 26, 2012

RAIS JK AMLETA DIAMOND KUWATUMBUIZA WANACHAMA WA CCM DMV


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kumpa jukumu maalum, Lady Detective inairusha hewani.
Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti’ alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.kwa sababu zisizo zuilika alishindwa kuwasili siku hiyo ya ufunguzi ila atawasili jumatatu na kuwatumbuiza wana CCM hao siku ya September 1.
“Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani.
“Kwa mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari,” alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins

No comments:

Post a Comment