Sep 19, 2012

AFARIKI DUNIA KWA KUJARIBU KUONGEZA UKUBWA WA NYETI ZAKE,,,,DUNIA haikaukiwi matukio ya kustaajabisha, kwa hakika huu ni ulimwengu maridhawa na hawakukosea walionena kwamba dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Stori ya kusikitisha, inatokea nchini Marekani ambako kijana Justin Street, amepoteza maisha akiwa kwenye jaribio la kuongeza ukubwa wa nyeti yake.
Habari kamili ipo hivi; Justin, 22, akiwa baba wa watoto wawili alikwenda kwa mwanamama Kasia Rivera ,35, aliyejitangaza kuwa ni mtaalamu wa tiba za kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume.
Kasia aliweka matangazo barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume, hivyo kumfanya Justin ahamasike kwenda kupata dawa hiyo ili kujiongezea ushababi.
Wanasema tamaa mbele mauti nyuma, ndivyo ilivyotokea kwa Justin, kwani baada ya kuomba dawa ya kuongeza ukubwa wa maumbile yake ya kiume, alidungwa sindano yenye madini ya silikoni.
Madini hayo, alidungwa kwenye nyeti yenyewe na baada ya muda mfupi, hali ya afya yake ilibadilika kuwa mbaya, alizorota na siku iliyofuata alifariki dunia.
Kutokana na tatizo hilo, Kasia alifikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji akituhumiwa kufungua zahanati bubu ndani ya nyumba yake iliyopo New Jersey, vilevile kutoa tiba za kiafya wakati hana taaluma hiyo wala leseni ya kuendesha kazi hiyo ya utoaji huduma za afya.
Kasia alipandishwa kizimbani wiki iliyopita, uchunguzi wa maiti umethibitisha kwamba Justin alifikwa na mauti baada ya madini ya silikoni aliyodungwa kwa sindano kuziba njia za mishipa ya damu.
Mmoja wa madaktari waliomfanyia uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kusikia silikoni inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya wanawake imetumika kwenye kuongeza ukubwa wa uume.Kasia, amekana kuhusika na mauaji hayo.

No comments:

Post a Comment