Sep 22, 2012

EDA SYLVESTER ATWAA TAJI LA REDD'S MISS TEMEKE, 2012


Redd's Miss Temeke 2012, Eda Sylvester akiwa katika pozi baada ya kutwaa taji lake usiku wa kuamkia leo.
Eda Sylvester (katikati) akiwa na mshindi wa pili Flaviana Maeda (kushoto) na mshindi wa tatu Catherine Masumbigana (kulia).
MREMBO Eda Sylvester usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kutwaa taji la Redd's Miss Temeke 2012 katika kinyang'anyiro kilichofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam. Eda Sylvester mwenye umri wa miaka 21 anatoka katika kitongoji cha Kigamboni na ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua Shahada ya Sanaa. Eda anapendelea kusafiri na kuangalia filamu. Matarajio ya mshindi huyo ni kuwa msanii wa kimataifa na mfanyabiashara mwenye mafanikio ya juu.

No comments:

Post a Comment