Sep 11, 2012

H BABA AJITAPA KUMGUNIKA DIAMOND,,,,MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Hamis Baba ‘H Baba’ amejitapa kumfunika mwanamuziki mwenzake ‘anaye-shine’ kinomanoma kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kimafanikio.
Akizungumza na kona ya Mbovu Mbovu za Mastaa juzikati jijini Dar, H Baba alisema muda wa Diamond kufanya vizuri umeshapita na sasa ni zamu ya wasanii kutoka Mwanza kuiteka Tanzania kwa mafanikio ya kimuziki.
“Yah sasa hivi ni zamu yetu, tazama kwa sasa ninavyowapeleka spidi kwenye anga zote. Muziki ninawakimbiza, uigizaji pia siko nyuma,” alisema H Baba. 

No comments:

Post a Comment