Sep 11, 2012

PHD SASA 'AMTAKA JACK WA CHUZI'



BAADA ya msanii wa filamu Jackline Pantezel ‘Jack wa Chuzi’, kuwatetea wanawake juu ya kuchukuliwa kama samaki na msanii Hemed Suleiman ‘P.H.D’ sasa staa huyo naye ameamua kufunguka na kudai kuwa hakupanga kutembea na mwanadada huyo lakini sasa ajiendae kutoka naye kwani amejipendekeza kwa kuzungumzia kauli yake.
Awali kabisa Hemed alidai kuwa endapo akiamua kuoa basi atafanya mchakato kama wa BSS wa kufanya mchujo na kupata yule mwanamke bora zaidi na mrembo kitu ambacho kilimfanya ‘Jack wa Chuzi’ kuinuka na kumtaka Hemed awaombe radhi wanawake kwani asiwachukulie kama samaki wanaopatika kilahisi tena kwa wingi.
Kauli hiyo ya Jack inaonekana kumtokea puani kwani mambo yanazidi kuwa magumu ambapo PHD anadai kuwa atafanya juu chini ili tu amuonesha Jack kuwa yale anayoyazunumza anauwezo wa kufanya na hata yenye anaweza kuwa mmoja kati ya wanawake watakaohitaji kuolewa naye ingawa hana vingezo anavyovihitaji.




“Sikupenda kauli ya Jack kwani namchukulia kama msanii mwenzangu ambaye nafanya naye kazi lakini kitendo chake cha kupinga kauli yangu kumenifanya niwe na hamu ya kutoka naye ili tu ajue kwamba nina uwezo wa kutoka na mwanamke yeyote tena pale ninapomuhitaji tu,” alidai Hemedi.
Hata hivyo mwandishi wa ishu hii baada ya kumtafuta muhusika wa pili wa kideo hiki Jack, alidai kuwa Hemedi hawezi kufanya kitu chochote kwake na anamchukulia kama mtoto anayekuwa na kuanza kujua wanawake hivyo haoni kama anaweza kuleta madhara.
“Hemed ni mtoto hivyo namchukulia kama ndo kwanza anawajua wanawake sasa, kwa sababu mtu mzima awezi kuanza kujisifu kuwa anaweza kurembea na kila mwanamke, kwani tayari ameshapitia huko asa kwa huyo ndo kwanza anawajua wanawamke siyo makosa yake anahaki ya kusema hivyo,” alisema Pentzel.

No comments:

Post a Comment