Sep 11, 2012

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA WAKUTANA, KUANZA MAANDAMANO SAA 3 ASUBUHI KESHO...Waandishi wa Habari wakiwa katika kikao kilichofanyika leo katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mbeya (MBPC) leo kujadili utaratibu wa maandamano ya wanahabari kesho.
Katibu Mkuu wa Mbeya Press Club, Kenneth Mwazembe akiongea na wanahabari wa mkoa wa Mbeya juu ya maandamano ya kesho.
Wanahabari wakifuatilia kikao hicho.
Waandishi wa habari mkoa wa Mbeya, kesho Septemba 11, 2012 wataungana na wanahabari wote nchini kufanya maandamano ya amani kupinga mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa na Mwandishi wa Habari wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi yaliyofanyika mnamo Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.
Maandamano hayo yatahusisha wanahabari wote mkoani Mbeya ambapo yataanzia eneo la Mafiati na kuishia katikati ya jiji la Mbeya eneo la BP jirani na ofisi za TRA mkoa wa Mbeya. Maandamano hayo yataanza saa tatu asubuhi.

No comments:

Post a Comment