Oct 22, 2012

BAADA YA KITAMBAA CHEUPE SASA NI CHUPI NYEUPE,,,,


Kitambaa cheupe ni kitambaa ambacho hung'aa vizuri sana na wanamuziki wamekuwa wakikitumia kama uniform, kama wanavyoonekana Wananjenje katika picha hii, na King Kiki alikipandisha shati kwa wimbo wake maarufu Kitambaa cheupe, ambapo alikuwa akiwahamasisha wapenzi wa muziki kutembea na kitambaa cheupe na kukiinua na kukionyesha wakati akiimba wimbo wake huo maarufu. Karibuni kumekuweko na maendeleo mapya ya kitambaa cheupe ambapo wanamuziki wabunifu wametumia kitambaa hicho kushona chupi ambazo nao kwa kutumia mtindo wa Mzee Kiki wameanza kuonyesha wapenzi wa muziki wao. Lady Detective anasubiri wanamuziki hawa kama nao watawahamasisha wapenzi wao wa muziki kuvaa chupi nyeupe na kuzionyesha wakati wanacheza kwa huu mtindo wao mpya ambao magazeti ya nanili yanadai unaitwa 'UNAKULAGA?" Mdau mmoja wa muziki alisikika akisema lazima nae ashone chupi nyeupe ili akaionyeshe kwenye show ijayo....je na sisi Tanzania tumegundua staili mpya itakayotingisha katika ulimwengu wa muziki duniani? Je chanel O watatupaisha au watatubania? Je Wanaijeria wataachana na Azonto wajitose kwenye huu mtindo mpya wa 'UNAKULAGA'?

No comments:

Post a Comment