Oct 24, 2012

BONGO NA REALITY TV SHOW,, WATAKOMAJEEE


JIDE KUIBUKIA KWENYE RUNINGA

Lady Jaydee azungumzia show yake ya TV na wasanii watatu anaowakubali Tanzania

Lady Jaydee katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango ambapo alipata nafasi ya kuongea kuhusu muziki na pia kuimba live. Katika kipindi alijibu maswali mengi ikiwepo kwa nini amechelewa kutoa album nyingine ambapo alijibu kuwa kwa sasa album hazifanyi vizuri sokoni kama zamani kutokana na kukithiri kwa wizi wa kazi unaofanywa na watu wanaouza CD feki na pia ku-burn CD. Swali la kwa wapi anapata inspiration ya kuandika nyimbo zake alisema nyimbo zake nyingi ni mambo yanayomzunguka kila siku huku akitolea mfano wa wimbo wa machozi akisema ulikuwa ni stori ya kweli iliyomtokea.
Pia aliongelea show yake ya reality iitwayo DIARY YA LADY JAYDEE kitakachokuwa kikiruka kupitia EATV.
Jaydee aliekuwa na mpiga kinanda wake alisema katika wasanii wa bongo fleva kwa sasa anawazimia Lina, Diamond na Barnaba.

No comments:

Post a Comment