Oct 31, 2012

VIINGILIO VYA FAINALI YA REDD’S MISS TANZANIA 2012 VYATANGAZWAMkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuanza kuuzwa kwa tiketi za shindano la Taifa la Redd's Miss Tz. Kushoto ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tz, Bosco Majaliwa.
FAINALI za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel,  Ubungo Plaza jijini D’salaam.
Akizungumza na waanmdishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema maandalizi yote yamekamilika na kila kitu kipo tayari na leo tupo hapa kuwatangazia Watanzania na washika dau wote wa tasnia ya Urembo kuwa tiketi kwa ajili ya shindano letu la mwaka huu zipo tayari na zipo kwa idadi maalum na leo hii zinaanza kuuzwa katika vituo tulivyovipendekeza kulingana na maoni ya wadau
Kutokana na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila tiketi itagharimu kiasi cha shilingi laki moja (100,000) za Kitanzania.
Katika kufanikisha shindano hili kutakuwa na vitu tofauti na miaka ya nyuma na tutarajie kuona shindano lenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya warembo wetu ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini
Vituo vinavyoanza kuuza tiketi hii leo ni. Stears samora
Regency Park Hotel, Rose Garden Mikocheni, Shear Illusion-Mlimani City, Giraffe Hotel, Ubungo Plaza na ofisi za Lino.
Nitoe rai kwa wapenzi wote waweze kupata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu kwa sababu ya kikomo cha tiketi kilichopo kama tulivyotangaza awali
Kwa upande wa burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii nguli hapa nchini kama:
1)    Diamond Platnumz
2)    Winfrida Josephat’Rachel’
3)    Wanne star ngoma troupe
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo yanayojulikana kama [Fast Tract] Tayari washiriki 5 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika kundi la Warembo 15 Bora.     [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni
               Lucy Stephano – Miss Photogenic
               Magdalena Roy – Top Model
               Mary Chizi – Top Sport Woman
               Babylove Kalalaa – Miss Talent
               City sports lounge-iliyopo posta mpya mkabala na mnara wa askari.
               Happiness Daniel – Miss Personality
Mwisho napenda kutoa shukrani zangu kwa wadhamini wetu ambao ni TBL kupitia kinywaji chao cha Redds Original,Star Tv na Giraffe Hotel    
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI

No comments:

Post a Comment