Jan 31, 2013


KATIBU MKUU WA UVCCM MARTIN SHIGELA ASHIRIKI SHUGHULI ZA KILIMO NA KUKAGUA MIRADI KIGOMA VIJIJINI

5 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM, UVCCM Bw. Martin Shigela akishiriki katika kupalilia shamba la Karanga katika kijiji cha Nkungwe Tarafa ya Mabembe Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembelea na kujionea shughuli mbalimbali na kukagua miradi inayotekelezwa na wananchi kwa pamoja na Serikali jana.
Sekretarieti ya CCM ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana iko mkoani Kigoma kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na sherehe za miaka 36 ya chama hicho zinazotarajiwa kufanyika Februari 3 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo, kulia ni Bi Fatma mmiliki wa na kushoto ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini.
3 
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nkungwe wakati alipotembelea katika kijiji hicho jana
4Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akikabidhiwa zawadi ya mihogo na Bi Asha Ibrahim mara baada ya kutembelea shamba lake jana, .Kijiji hicho cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha muhogo bra katika mkoa wa Kigoma.
8Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akiongozana na Bw.Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini mbele yake wakati akikagua shughuli za ukulima wa kisasa katika kijiji cha Nkungwe Kigoma Vijijini, Kijiji hicho cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha muhogo bra katika mkoa wa Kigoma.
9Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimsaidia Bi. Asha Ibrahim kufukia mbegu ya Viazi, huku viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Kigoma Vijijini wakishuhudia tukio hilo.7 Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimkabidhi zawadi ya shilingi elfu 10,000 mtoto Rehema huku mama yake akimsaidia wakati alipotembelea na kujionea shughuli za kilimo katika kijiji cha Nkungwe jana
11 Viongozi mbalimbali wakikagua kivuko cha Mto Ruchi katika kijiji cha Nkungwe jana.
12Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akivuka katika kivuko cha Mto Ruchi kwa kutumia Baiskeli huku akiwa ameonozana na viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Kigoma Vijijini pamoja na watendajiwa kijiji hicho jana inaelezwa kwamba watu wengi walipotea maisha kwa kuliwa na Mamba kabla ya kujengwa kivuko hiki.
13Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimenya muhogo ili kutafuna kidogo mara baada ya kununua kwa mmoja wa wakulima Kijiji cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha Muhogo mkoani Kigoma
15Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akiagiza jambo kwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kigoma Bw Peter Msanjila wakati alipotembelea kata ya Mwanduga jana kulia ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini
16Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kabanda katika kijiji cha Chabwimba jana
18 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili katika Kata ya Mabembe.
19Wananchi wa kijiji cha Mabembe wakimsikiliza mwenyekiti wa UVCCM katika Kata ya Mabembe kwenye mkutano wa ndani
20Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akicheza na msanii chipukizi wa kijiji cha Mabembe ambaye ni mlemavu wakati alipotembelea na katika Kata ya Mabembe
23 Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kata ya Mwanduga Kigoma vijijini jana
24Mjumbe wa NEC CCM kupitia Wilaya ya Uvinza Asha Baraka akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mwanduga Kigoma jana kulia ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Kigoma Vijijini na katikati ni Peter Msanjila Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kigoma.
25Martin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye kata ya Mwanduga Wilaya ya Kigoma vijijini
26Matin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akipata maeleo kutoka kwa Khamis Bitese Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembele na kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya Kabanda.
27Martin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akipata maeleo kutoka kwa Khamis Bitese Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembele na kukagua ujenzi wa numba za walimu katika shule ya msingi ya Kabanda.

No comments:

Post a Comment