Mar 15, 2013


UCHAGUZI CCM DMV, WAINGIA DOA, WAOGOMBEA 6 WAJIENGUA

Wagombea sita wamejitoa katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa CCM DMV uchaguzi utakaofanyika kesho Jumamosi March 16, 2013 kwenye Address ya 500 Sligo Ave. kuanzia saa 9 alasili (3pm) ET.

waliojitoa kwenye uchaguzi huo ni Mrisho Mzese aliyekua anagombea nafasi ya Mwenyekiti, Al Amin Hassan Chande Othman aliyekua akigombea nafasi ya Mwenyekiti wa Vijana, Steven Ngosha aliyekua akigombea nafasi ya Katibu Mwenezi na Itikadi, Warashi Khamisi na Ismail Abubakar Mwlima waliokua wakigombea nafasi ya Halmashauri Kuu ya Tawi na Fadhili Londa aliyekua akigombea nafasi ya Katibu wa Vijana.

Sababu kubwa ya wagombea hao sita kujitoa ni kuwa na wasiwasi wa kupanga matokea na kujiunga kwao na CCM DMV na hatimae kugombea ni mapenzi yao na chama lakini wanaona matatizo tangia kwenye kamati ya uchaguzi mpaka kwenye uchaguzi wenyewe na kusema kuna wagombea wanaotakiwa kushinda na sio wao ndio maana tumeamua kujitoa.

Tangia uchaguzi huu utangazwe kumetokea wingi wa wanachama wapya waliotaka kujiunga na chama na wachunguzi wa mambo wanasema sababu ni kutaka kuuondoa uongozi wa muda  uliokuwepo madarakani lakini katika uchaguzi utakaofanyika hiyo kesho ni kiongozi mmoja tu aliyekua kwenye uongozi wa muda anayegombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama.

Vijimambo ilimpigia simu mmoja wa wanakamati ya uchaguzi kujua kulikoni nae alisema kujitoa kwa wagombea, habari hizo nae amezisikia mitaani wagombea hawajaiandikia barua kamati lakini cha msingi ni kwamba kunapotokea wagombea wawili ni lazima aibuke mshindi sasa kama wewe unaona utashindwa uchaguzi na kuamua kujitoa na bila kufuata taratibu na kuamua kupeleka taarifa kwenye vyombo vya habari kujitoa kwako basi kiongozi huyu anatatizo na kitu kingine Viongozi hawa waliojitoa walikua wanataka wapewe kadi za kuandikisha wanachama na taratibu za chama zilivyo wanachama wapya husajiliwa na uongozi na si mgombea.
( Habari kutoka Vijimambo)

No comments:

Post a Comment