Apr 17, 2013

HII NDIYO AJALI YA WANAFUNZI WA ST. CHARLES ILIYO TOKEA MJINI IRINGA



Wasamaria  wema  wakitoa msaada kwa  wanafunzi  wa shule ya St Chalresy Iringa  waliojeruhiwa katika ajali  leo 










Wanafunzi  waliojeruhiwa katika ajali  wakilia kwa uchungu kabla ya  kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa 









Wanafunzi hao  wakiwa  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa 

Askari  wa usalama barabara  wakifika eneo la  tukio  kutoa msaada  

Wanafunzi hao  majeruhi  wakiwa  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa

Askari  wa  usalama barabarani akitoa msaada  kwa  majeruhi  wanafunzi  wa St. Chalresy leo katika Hospitali ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa 







WANAFUNZI  zaidi ya 20  wa shule  ya  kimataifa ya  St Charles iliyopo  Don Bosco katika Manispaa ya Iringa  wamenusurika  kifo  baada ya  gari  waliyokuwa  wamepanga aina ya Daladala lenye namba T415  AEG kushindwa  kupanda mlima na kupinduka.
Huku mbinu  za  wezi  wa  watoto  zikionyesha  kugonga mwamba baada ya  mwanamke mmoja  kushtukiwa akitaka kukimbia na mtoto  asiye wake kwa madai anamkimbiza Hospitali.

Ajali  hiyo  imetokea majira ya saa 2 mchana  wa  leo  katika  eneo la Msikiti  wa Hidaya katika  kata ya Mvinjeni katikati ya mji  wa Iringa.


Wakizungumza na  mwandishi  wa habari  hizi  eneo la  tukio  baadhi ya mashuhuda  walisema  kuwa daladala  hilo ambalo lilikuwa  likitokea  eneo la Frelimo katika Manispaa ya Iringa  kuelekea mjini Iringa mara baada ya kufika  eneo hilo lilishindwa  kupanda  mlima na kuanza  kurudi  nyuma kwa kasi kabla ya kupinduka.


Alisema  shuhuda  huyo Juma Omari  kuwa chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ,ubovu  wa gari hilo pamoja  na uzembe wa  dereva ambaye  alionekana  kuendesha gari hilo kwa bila  kuchukua tahadhari na pamoja na  kutambua mbele  kuna kona na mlima ila hakuweza  kuzingatia  hilo.


Hata  hivyo  alisema  kutokana na ajali  hiyo  dereva  na konda wake  waliwatelekeza   watoto hao ambao  wanakadiliwa  kuwa na umri  wa miaka 7 na 9 na  wao  kutoweka  kusikojulikana na kuwaacha  watoto hao bila kuwapa msaada  wowote hadi wananchi  walipofika  kutoa msaada  wa  kuwatoa katika daladala  hilo na  kuwakimbiza  katika  Hospitali ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa kwa matibabu  zaidi .


Alisema  katika ajali  hiyo hakuna aliyepoteza maisha  zaidi ya mwanamke mmoja ambae jina  lake bado kufahamika  aliyejeruhiwa  vibaya  mikono  yake.


Hata  hivyo  mmoja kati ya wauguzi  wa Hospitali ya mkoa  wa Iringa ambae  hakutaka  kutaja  jina lake kwa kuwa  si msemaji  wa Hospitali  hiyo alisema  kuwa hali  za  watoto hao  si mbaya  sana  zaidi ya  kupata michubuko midogo midogo .


Diwani  wa kata ya Mvinjeni Frank  Nyalusi amethibitisha  kutokea kwa ajali  hiyo na  kuwapongeza  wananchi  wa kata  hiyo ambao  walifika  kutoa msaada kwa  watoto  hao kwa kuwakimbiza  Hospitali.

wakati  huo  huo mwanamke mmoja ambae  jina halikuweza kupatikana mara moja amedaiwa  kutka  kuiba mmoja kati ya  watoto  waliojeruhiwa kwa madai  kuwa ni mtoto  wake na alikuwa akitaka  kumkimbiza Hospitali ya wilaya ya Iringa Frelimo badala ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa ambako majeruhi  wengine  walikimbizwa .

Mwanamke  huyo alishtukiwa baada ya  kukutwa akitimua mbio uchochoroni huku akiwa na mtoto  huyo na baada ya kubanwa aliamua  kumtelekeza mtoto  huyo na kukimbia hali iliyopelekea uongozi  wa mtaa kuomba watoto  wote  wale  waliojeruhiwa na wazima kukimbizwa  Hospitali ya mkoa .

No comments:

Post a Comment