OPARESHENI DHIDI YA ‘BODABODA’ ZENYE MAKOSA YAPAMBA MOTO MORO
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Morogoro, Leonard Gyindo (kulia), akipokea maelezo kutoka kwa askari aliyepewa jukumu la kuandikisha pikipiki zilizokamatwa.
JESHI la polisi mkoa wa Morogoro leo limeanza zoezi la kukamata pikipiki 'bodaboda' zenye makosa mbalimbali yakiwemo ya madereva na abiria kutovaa kofia ngumu.
Akizungumza na mtandao huu, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro (RTO) Leonard Gyindo, amesema kabla ya kuanza kwa oparesheni hiyo walifanya mkutano na madereva na wamiliki wa bodaboda hizo.
Katika hali ya kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo, askari kanzu wamekuwa wakifanya kazi hiyo badala ya wale wa FFU wanaotumia pikipiki ambapo madereva wengi wa bodaboda wamejikuta wakikamatwa kirahisi.
No comments:
Post a Comment