Jul 27, 2012

BONGO NA WASANII LEO.......

ATOA WOSIA KWA RAFIKI ZAKE " SIKU YA KIFO CHAKE"
MKONGWE wa sanaa ya maigizo nchini, Jacob Steven ‘JB’ ametoa wosia kwa rafiki zake ambao watatakiwa kuufuata siku atakapolala katika nyumba yake ya milele. Akizungumza na reporter wetu hivi karibuni jijini Dar, JB alisema neno la mwisho ambalo atapenda rafiki zake walizingatie ni kushikamana na Mungu aliye hai na kuwa na toba kila iitwapo leo. “Hakuna ajuaye siku ya kufa kwake. Wakati wowote nikiondoka duniani nitapenda rafiki zangu wote washikamane na Mungu na kuwa na toba ya kweli kila kukicha ili nao siku moja waje kuurithi uzima wa milele,” alisema JB. Pamoja na wosia huo kwa rafiki zake, JB amewataka wasanii wenzake kuwa wacha Mungu siku zote ili pale umauti utakapowakuta wawe na tumaini la kuwa na maisha mazuri baada ya kifo. Kutoka kwa George Kayala...

No comments:

Post a Comment