Jul 27, 2012

ASEMAVYO JACQUELINE DUSTAN "Jack"

WANAUME WAMEDATA NA VINGI KWANGU........
MSHIRIKI wa Maisha Plus season 11, Jacqueline Dustan ‘Jack’ ambaye anajikongoja kwenye tasnia ya filamu amefunguka kuwa wanaume wanamtolea macho na kudata na vitu vingi vilivyopo mwilini mwake kutokana na kujengeka vyema. Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Jack alisema kuwa anajijua kuwa ni mrembo na wanaume wanadatishwa na umbile lake lenye mvuto lakini hawezi kukubali ombi la kila mmoja kwa kuwa anajiheshimu. “Siyo kila mwanaume lazima nitoke naye kwa kuwa miye ni mzuri, ninajilinda na kujiheshimu hadi nitakapompata mwanaume mmoja wa maisha yangu na kufunga naye ndoa,” alisema. Jack aliongeza kuwa vishawishi anavyokumbana navyo ni vingi lakini kwa kuwa anajitambua kuwa ni mrembo atafanya jitihada zote kuhakikisha anavishinda ili asiharibiwe na wanaume wakware.

No comments:

Post a Comment