Jul 13, 2012

MAMA WA MAREHEMU KANUMBA ALAZWA ZAHANATI MANZESE

MAMA mzazi wa marehemu Steven Charles Kanumba, Flora Mtegoa juzi alilazwa katika Zahanati ya Kilimani, Manzese jijini Dar kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu pamoja na Malaria. Chanzo chetu kilichopo hospitalini hapo kilisema kuwa, mama huyo alifikishwa katika zahanati hiyo usiku wa Julai 9, mwaka huu huku akiwa hoi. “Mama Kanumba hakutaka kwenda kwenye hospitali nyingine yoyote zaidi ya kwenda kwa daktari aliyekuwa akimtibia mwanaye maarufu kwa jina la Kidume ambaye anafanya kazi katika zahanati ya Kilimani,” kiliendelea kusema chanzo hicho. Baada ya kupata taarifa hizo, paparazi wetu alitinga katika zahanati hiyo ili kuhakikisha kama kweli mama huyo alikuwa amelazwa, alipofika nje aliliona gari la marehemu Kanumba na alipoingia ndani alimuona mama huyo. Hata hivyo, jitihada za kupata picha yake akiwa kitandani zilishindikana kutokana na mazingira kutoruhusu. Aidha, The fashion detective iliongea na mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco ambaye alikiri mama yake kulazwa katika zahanati hiyo. “Ni kweli mama amelazwa na anasumbuliwa na malaria pamoja na presha, anaendelea kupata matibabu,” alisema Seth.

No comments:

Post a Comment