Jul 13, 2012

SAUTINYA RADI AKUTWA HOI GUEST HOUSE

RAPA maarufu wa Bendi ya Mashujaa, Nick Noah ‘Sauti ya Radi’, juzi alikutwa hoi ndani ya gesti ya Malindi alipofikia baada ya kutua mjini hapa akiwa na bendi yake kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la ZIFF. Kwa mujibu wa chanzo chetu, msanii huyo alikutwa ndani ya chumba kimoja cha gesti hiyo majira ya mchana akikoroma ambapo alipoamshwa alionekana kama mtu aliyetaka kukata roho. “Yeye na wenzake waliingia vyumbani mwao saa 3 asubuhi, wengine wakatoka kwenda kuzunguka lakini yeye alibaki ndani, sasa akiwa chumbani sijui alipatwa na kitu gani, mmoja wa wasanii wenzake alipoingia akamkuta anakoroma. “Jitihada za kumpa huduma ya kwanza zilifanyika na baada ya muda akarudi kwenye hali ya kawaida licha ya kwamba alikuwa na mawenge flani,” alisema mtoa habari huyo. TFD (The Fashion Detective)lilimtafuta rapa huyo na alipopatika alisema: “Unajua huwa sipendi safari za majini kwa kuogopa mambo haya, vile tumesafiri na meli ndiyo haya yamenikuta.” Lakini sasa hali yake ni nzuri na anaendelea na maisha kama kawa....

No comments:

Post a Comment