Jul 25, 2012

NDANI YA CHADEMA LEO.

CHAMA   cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepokea  wanachama wapya 256 kutoka vyama vya CCM, Cuf, na TLP kutoka katika Kata nne za Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Hayo yalibainishwa na Katibu wa Chama hicho  Wilaya ya Kilombero , Moses Kisenime katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari. Kisenime alisema wanachama hao walipokelewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Bavicha), John  Heche wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara  jimboni humo. Alisema Mwenyekiti huyo wa Bavicha taifa aliwapokea wanachama hao katika mikutano minne aliyofanya katika Kata ya Ifakara, Mang’ula, Msolwa na Mkamba. “Kutokana na mikutano yetu tunayoifanya mkoani Morogoro tumeweza kupokea wanachama  214  kutoka CCM, Cuf 28 na TLP wanachama 14,” alisema Kisenime. Akizungumza kwa niaba ya wenzake  aliyekuwa balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mkamba, Mussa  Katanduki alisema ameamua kuhama kutoka chama cha CCM  kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mueleko na maadili ya uongozi. “Sijalazimishwa na mtu kuhamia Chadema lakini kutokana na mambo yalivyo ndani ya CCM kwa ihari yangu nimeamua kuungana na chama hiki ili kuweza kuendeleza mapambano ya kutetea haki za wanyonge,” alisema Katanduki.

No comments:

Post a Comment