Jul 16, 2012

SHILOLE CHUPUCHUPU KUVULIWA NGUO BARABARANI.

MSANII wa filamu na muziki wa Pwani, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameponea chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani maeneo ya Darajani mjini hapa baada ya kukatiza mitaa ya sokoni akiwa katupia kigauni kifupi ajabu. The Fashion Detctive (T.F.D)ilimshuhudia Shilole akiwa na wanenguaji wake akipigiwa kelele na wanaume waliotaka kumkamata wamvue kisha wamlambe viboko hivyo akalazimika kukimbilia dukani akanunua dira na kulivaa juu ya kigauni cha kihasara alichokuwa amekitinga.

No comments:

Post a Comment