Aug 10, 2012

BASI LA KAMPUNI YA SABENA LAUA WATU 17...


BASI LA KAMPUNI YA SABENA LILIPO PINDUKA NA KUUWA WATU 17 
Basi la Sabena linavyoonekana baada ya kupinduka. 
MAJERUHI WANNE WA AJALI YA BASI LILILOPINDUKA HALI ZAO MBAYA, POLISI WANASEMA LILIKUA LIMEBEBA ABIRIA ZAIDI YA 110 WAKATI LIKIPINDUKA NA KUUA WATU 17, HUKU MAJERUHI WAKIWA 78.... AMBAPO MAITI SABA ZINATARAJIWA KUTATAMBULIWA NA NDUGU ZAO ... 
Abiria wanne kati ya majeruhi 78 walioumia katika ajali ya basi la Kampuni ya Sabena lililopinduka mkoani Tabora, hadi sasa wako katika hali mbaya huku abiria 17 wakithibitika kufariki dunia. 

Basi hilo aina ya Scania, lenye namba za usajili T 570 AAM, lilipinduka juzi mishale ya saa 6:30 mchana katika eneo la Kitunda, wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Akizungumzia ajali hiyo leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Anthony Rutta, amekaririwa akisema kuwa basi hilo lilijaza abiria kupita kiasi na kwamba, wakati likipinduka, ndani yake lilikuwa na abiria zaidi ya 110.

Majeruhi waliobaki bado wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Kitunda na jitihada za kuwahamishia katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora ya Kitete zinaendelea, lakini abiria 54 waliruhusiwa na kuendelea na safari yao.

Hadi kufikia leo, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa, ambao ni askari Polisi PC Kheri wa Kituo Kikuu Kikuu cha Polisi cha mjini Tabora, Vitus Tulumanye, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) tawi la Tabora; Farah Inga; raia wa Zimbabwe aliyekuwa akifanya kazi Tabora; Ikamba Thadeo; Damalu Goma; Beatrice Kalinga, mwalimu wa Shule ya Msingi Igoko wilayani Uyui mkoani Tabora na aliyetambuliwa kwa jina moja la Madirisha ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi katika Wilaya ya Kaliua.

No comments:

Post a Comment