Aug 20, 2012

DIVA AJITAPA KUGOMBEA UBUNGE 2015
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Radio, Loveness Malinzi ‘Diva’ amejitapa kuwa mwaka 2015 lazima agombee ubunge kwenye Jimbo la Kigoma Kaskazini akiamini atashinda.
Kupitia blog yake mwanadada huyo amedai kuwa anajua kwa kutangaza nia huko wapo watakaodhani anatania lakini ukweli ni kwamba amedhamiria.
Alisema: “Nataka 2015 nikagombanie Ubunge Kigoma, swali ni je, kugombania ubunge Kigoma ni lazima niwe mzawa wa Kigoma? I love Kigoma na nitashinda.
“Nitatumia njia inayoitwa strength of a woman (nguvu ya mwanamke).
Kwa nini nataka kugombea Kigoma na siyo sehemu nyingine? Ni kwa sababu watu wa huko ni wazuri, wacheshi, wana heshima na wanakubali cha kwao.”
Licha ya maelezo yake hayo, bado kuna ambao hawaamini kama kweli amedhamiria huku wakidai eti hayo ni maneno tu, hata kwenye kanga yapo.

No comments:

Post a Comment