Aug 29, 2012

MAMBO YA BUNGE LA KENYA NA BAJETI ZAKE

KITI KIMOJA CHA MBUNGE CHAGHARIMU SHILINGI MILIONI NNE! 

KITI cha mbunge wa Kenya anachokalia akiwa bungeni kina thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 4 ( sh. za Kenya ni  200,000).
Wakati kiti kimegharimu kiasi hicho cha fedha, ukarabati wa jengo la bunge la Kenya umegharibu shilingi za Kitanzania  bilioni 18.4 ( sh. za Kenya ni milioni 920), fedha ambazo zimelalamikiwa na wananchi wa nchi hiyo ambao wamedai kuwa ni nyingi mno na wakadai kuwa  huo ni ufisadi mkubwa.
Hata hivyo, Spika wa Bunge la Kenya, Kenneth Marende  (pichani)amesema: “Kiasi hicho cha fedha zilizotumika siyo kikubwa kama watu wanavyofikiria kwa kuwa viti hivyo ni vya kipekee, hata malighafi iliyotumika kutengenezea ni tofauti na vingine.” Ukumbi huo wa Bunge la Kenya unafanana na ule wa Bunge la Tanzania na Ujerumani.

No comments:

Post a Comment