Aug 29, 2012

MUZIKI NA BONGO

BELA KUFANYA WIMBO NA KAPTENI KOMBA


MLIMBWENDE aliyeibukia kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bela’ ameweka plain azma yao ya kutaka kushirikiana na mwimbaji mkongwe, Kapteni John Damian Komba.
Akizungumza kwa niaba ya memba wenzake wa kundi lao linalofahamika kama Scorpion Girls, Bela alisema baada ya kukamilisha video ya wimbo wao wa Watuache, sasa wameanza mazungumzo na Kapteni Komba ili wamshirikishe kwenye singo yao ya pili.
“Yule sisi ni kama mlezi wetu, tumeshamuomba na ameonesha moyo wa kutaka kufanya kazi na sisi na kutuambia tujipange kwa ajili ya kuingia studio kurekodi naye wimbo wetu wa pili,” alisema Bela.

No comments:

Post a Comment