Sep 4, 2012

RAIS JK KUTETA NA WAKUU WA TROIKA


RAIS Jakaya Kikwete, leo atakutana na wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa dhumuni la kuzungumzia mgogoro wa Jamuhuri wa Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mkutano huo wa siku moja utafanyika leo jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa wajumbe watakaoshiriki katika mkutano huo watatoka nchi za Msumbiji, Namibia pamoja na Tanzania.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa asasi za Troika ameitisha mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi hizo, ambao ni wajumbe wa asasi kwa lengo la kutadhmini hali halisi iliyopo ya mgogoro wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo”, ilisema taarifa hiyo.
Hata hivyo ilichanganua kuwa wakuu wa nchi hizo watawasili nchini kuanzia jana, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment