Oct 3, 2012

AUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI KATIKA AJALI YA MBALIZI MKOANI MBEYA     Kijana aliyedaiwa kuwa kibaka akiwa mikononi mwa wananchi waliofika eneo la ajali, Mbalizi mkoani Mbeya jana.

...akianza kushushiwa kichapo....akizidi kusulubiwa....kichapo kikiwa kimepamba moto....kijana huyo akiwa hoi kabla ya kukata roho. UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni, huo ndio msemo pekee ambao naweza kuutumia katika kukujuza yaliyotokea jana mchana katika ajali mbaya ya Mbalizi , Mbeya Vijijini. Wakati wengine wakiendelea kuokoa majeruhi, wengine wamejikuta wakifanya tofauti na vile ilivyotegemewa pale kijana mmoja alipojitoa mhanga na kuingia katika mmojawapo wa waokoaji na kutaka kumchomolea fedha.Dhahama ilimfika kijana huyo ambaye hakufahamika jina mpaka mauti yanamkuta, baada ya kukwidwa na mashuhuda wa ajali hiyo na kupewa kichapo cha mbwa mwizi.

No comments:

Post a Comment