Oct 3, 2012

AUNT LULU AGEUZWA DARAJA LA WANAUME ,,,,


Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’.

STAA wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ ametoa la moyoni kuwa, anaumizwa na kitendo cha baadhi ya wanaume kumtumia kimwili kisha kumtosa.

Akizungumza kwa masikitiko hivi karibuni, Aunty Lulu alisema yeye ni mwanamke anayehitaji mpenzi mwenye nia ya kumuoa lakini anashangaa kila anayekuwa naye anamtumia kama daraja kisha akifanikisha mambo yake anampotezea.
“Wananifanya mimi ni daraja. Wanapita kwangu ili kufikia malengo yao, wakiona wamefanikiwa wanaanza chokochoko ili tuachane, inaniuma sana,” alisema Aunty Lulu.

No comments:

Post a Comment