Oct 22, 2012

JAMANI INASIKITISHA SANA TUMSAIDIE MTOTO HUYU,,,,,


MTOTO YATIMA AANGUKIA MOTO, AUNGUA USONI

Mwandishi wetu Iringa
MTOTO yatima, Juliana Inuka, mkazi wa Kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa, mkoani Njombe ameungua vibaya usoni baada ya kuangukia moto.
Mtoto yatima, Juliana Inuka
Mwandishi wetu Francis Godwin alimshuhudia mtoto huyo katika kijiji hicho akiwa katika hali mbaya na alielezwa na wananchi kuwa aliungua zaidi ya mwezi mmoja uliopita na hakuwa anapatiwa matibabu kutokana na hali ya ufukara wa mtu anayeishi naye.
Hata hivyo, mwandishi huyo alifanya jitihada za ziada kwa kuchangisha michango ya fedha na kufanikiwa kumfikisha Juliana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako anapatiwa matibabu.
Akizungumza na gazeti hili, Godwin alisema aliambiwa kuwa mtoto huyo ana ugonjwa wa kifafa, hivyo siku ya tukio ambayo hakuweza kuikumbuka aliangukia moto uliosababisha aungue usoni na mbaya zaidi alikaa nyumbani miezi saba bila kupata matibabu.
“Kuna baadhi ya watu vijijini wana hali mbaya sana, kielelezo tosha ni huyu mtoto ambaye ameungua vibaya, nawashukuru sana wasamaria wema waliomchangia na kutuwezesha kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako sasa hali yake inaridhisha kidogo baada ya kupata tiba,” alisema Godwin.
Alitoa wito kwa watu walioguswa na habari ya mtoto huyu kuendelea kumchangia ili kunusuru maisha yake kwa kutuma michango yao kwa njia ya M- Pesa namba 0754026299 au Tigo Pesa 0712 750199 ambazo ni za mwandishi huyo anayeratibu matibabu yake.

No comments:

Post a Comment