Oct 10, 2012

MAKAMU WA RAIS DK BILAL AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA UGANDA


Rais Yoweri Museveni wa Uganda akimkaribisha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye  sherehe za maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala,Uganda.
Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gaharib Bilal (kulia)  akibadilishana mawazo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 yaUhuru wa Uganda. Sherehe hizo zimefanyika jana katika Uwanja wa Kololo jijini Kampala. Wanaoonekana nyuma yao  ni wake zao, Bibi Janneth Museveni (kulia) na Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe  Mama Zakia Bilal wakifuatilia  matukio  mbalimbali  wakati wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda kwenye Uwanja wa Kololo, jijini Kampala  jana. Wengine kutoka kushoto ni Rais wa Somalia Hassan Shekhe Mahamoud  na Makamu Rais wa Sudan, Bwana  Haji Adam Yusufu.

No comments:

Post a Comment