Oct 25, 2012

MZEE WA DUSHELELE,, MAMBO YA DOLA HAYO... WATAKUWEZAJEEE,,,,???


HAYA NDIYO MALIPO YANGU KWA SHOO

Kama utakuwa msikilizaji mzuri wa xxl basi haina shaka kuwa utakuwa unakumbuka kwamba siku chache zilizopita Diamond Platinumz alitangaza kuwa analipwa kiasi cha shilingi milioni 8 kwa shoo moja ndani ya Tanzania.
sasa taarifa iliyopo ni kuwa ALLY KIBA ametangaza kuwa kwa sasa atakuwa akipiga dili ya shoo kwa kwa kiwango cha kimataifa cha malipo
Akizungumza na Lady Detective mapema leo nyota wa dushelele ali kiba amefunguka kuwa kwa sasa anapiga shoo shilingi za kibongo zaidi Milioni 12 ambazo ni sawa na dola 8000 za kimarekani kwa shoo zote za nje ya nchi na pia shilingi milioni 8 kwa shoo za ndani ya bongo.
"mara nyingi huwa sipendi kusema lakini ni kuwa kwa sasa nina ratiba kibao za shoo nje ya bongo na ambazo tayari malipo yake ni dola 8000 za kimarekani na hapa bongo nitakuwa napiga kwa kiwango tofauti ingawa sitapenda kushuka chini ya milioni 8" alisema Kiba

No comments:

Post a Comment