Oct 8, 2012

NDANI YA UVCCM,,,,


REHEMA MBEGU KAMWE (Mrs Bigright) kulia akiwa na kiongozi mwenzake wa UVCCM, Bi. MWANAFATMA RUBAI katika viwanja vya Karimjee wakati wa mkutano wa mkoa jana.
Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) kata ya Makumbusho na Ofisa Mahusiano wa Bigright Promotions, Bi. Rehema Mbegu ambae mara nyingi yupo na vijana katika michezo na shughuli za kijamii na mwenyekiti wa Garden Sports Centre amesema sasa hivi anaamua kujitosa mzima mzima na mambo ya siasa kwa kugombea nyadhifa zilizo katika chama akianzia wilayani. Haya ni kwa mapenzi yake ya chama na kuhakikisha hawatetereki katika kata yake na wilaya ya Kinondoni kiujumla katika chaguzi zijazo na kuleta maendeleo ya kweli katika mkoa wa Kinondoni na taifa kiujumla. Michezo ina nafasi yake na siasa ina nafasi yake hivyo nitaendelea kusaidiana na vijana katika michezo kama kawaida.

No comments:

Post a Comment