Oct 8, 2012

AJIPAKA KINYESI KUWAKWEPA POLISI MAHAKAMA YA KISUTU


Askari wa Jeshi la Polisi wakijihami na matambara pamoja na mifuko ya nailoni ili kumdhibiti mtuhumiwa aliyejipaka kinyesi mwili mzima na kutaka kuwakimbia askari kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja alidaiwa kuwa ni mwizi wa simu lakini hakimu alimwachilia huru kutokana na kukosekana ushahidi hata hivyo askari waliendelea kumshikilia tena jambo ambalo lili muudhi na aliporudi mahabusu aliamua kujipaka kinyesi mwilini.
Askari wakimdhibiti mtuhumiwa huyo kwa kutumia matambara na mashuka mazito kutokana na kuwa na kinyesi kingi.
Akipandishwa kwenye gari la polisi na kuondoka nae.
Akilazimishwa kuvaa nguo.
Akiondolewa eneo hilo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

No comments:

Post a Comment